Kategoria: Habari
Habari za hivi punde kuhusu matukio ya ndani na nje ya nchi, zikiangazia siasa, jamii, na masuala muhimu yanayoathiri maisha ya watu.
-

“Nitajizulu”: Waziri wa Nishati Zanzibar Atoa Kauli Katika Bunge la Wawakilishi
Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Nadir Alwardy amesema yuko tayari kujiuzulu iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake na kuwatumikia wananchi ipasavyo. Kauli hiyo ameitoa leo Mei 29, 2026 ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji, Nishati na Madini, huku akikiri kuwa wizara hiyo ni miongoni mwa wizara ngumu…
-

WHO Yaonya Ebola Kongo Inaweza Kusambaa Zaidi Afrika Mashariki
Shirika la Afya Duniani WHO limesema mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huenda ulianza takribani miezi miwili iliyopita kabla ya kuthibitishwa rasmi. WHO imesema tathmini ya ukubwa wa maambukizi pamoja na namna ugonjwa huo ulivyosambaa ndiyo imewafanya kufikia hitimisho hilo. Hadi sasa watu zaidi ya 130 wamefariki dunia kutokana…
-

Msanii Mkongwe wa Filamu Tanzania Hashim Kambi Afariki Dunia Jijini Dar es Salaam
Msanii mkongwe wa filamu Tanzania Hashim Kambi amefariki dunia Dar es Salaam baada ya kuzidiwa ghafla akiwa kazini, huku akidaiwa kusumbuliwa na presha na kisukari.
-

Serikali ya Tanzania Yajenga Mabanda 200 ya Wafanyabiashara Wahanga wa Moto Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Wakili Albert Msando, amesema wamefanikisha kujenga mabanda mapya ya wafanyabiashara zaidi ya 200 katika Soko la Mawasiliano (Simu 2000) ikiwa zimepita wiki tatu tu tangu soko hilo liungue moto. Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Msando amesema, “Hapa nipo Soko la Mawasiliano (Simu 2000). Soko letu baada ya kuungua tulipewa maelekezo…
-

JWTZ Yatangaza Nafasi Mpya za Kuandikishwa Jeshi, Yataja Vigezo Na Masharti
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi mpya za kuandikishwa kwa vijana wa Kitanzania, likieleza sifa, utaratibu wa maombi na muda wa kuwasilisha. Tangazo hilo limetolewa na Kevin Baraka Byabato, Luteni Kanali na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Uhusiano katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Akizungumza kwa niaba…
-

Mfanyabiashara Apatikana Ameuawa Ndani ya Gunia Kenya, Watu Wanne Wakamatwa
Mfanyabiashara mmoja kutoka Scotland (Uskochi) amepatikana akiwa ameuawa nchini Kenya, mwili wake ukiwa umefungwa na kuwekwa ndani ya gunia, huku polisi wakiwakamata watuhumiwa wanne katika tukio linalodaiwa kuwa ujambazi uliogeuka mauaji. Marehemu aliyetambuliwa kama Campbell Scott alikuwa amesafiri kwenda Nairobi kuhudhuria mkutano wa kibiashara kabla ya kupotea. Mwili wake ulipatikana baadaye ukiwa umetupwa katika eneo…
-

Mbunge Kangi Aibana Serikali kwa Mada ya Rushwa, Amtaka Waziri Mkuu Kuchukua Hatua
Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola, ameibua mjadala mkali bungeni baada ya kumtaka waziri mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba kuchukua hatua madhubuti dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoendelea nchini. Akichangia bungeni katika Dodoma Aprili 8, 2026, Lugola alisema licha ya kauli za mara kwa mara za serikali kuhusu kupambana na rushwa, bado hali halisi haionyeshi mabadiliko…
-

Mbunge wa Zamani Kilwa Kusini ‘Bwege’ Afariki Dar es Salaam
Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Said Bungara maarufu “Bwege,” amefariki Jumatatu mchana jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo katika hospitali binafsi.
-

Meli ya tatu ikielekea Dubai yatia nanga bandari ya Lamu kwa sababu ya vita ya Iran
Meli kadhaa za kubeba magari zimeanza kubadili safari na kuelekea Bandari ya Lamu nchini Kenya, kufuatia kuongezeka kwa hatari za usalama katika Mlango wa Bahari wa Hormuz. Hatua hiyo imeathiri moja kwa moja usafirishaji wa kimataifa, huku angalau meli tatu zikiripotiwa kufika Lamu baada ya kushindwa kuendelea na safari kuelekea Mashariki ya Kati. Moja ya…
-

Mwanamke Tanzania ashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mumewe kwa panga
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50, anayefahamika kwa jina la Maselina Mtewele, anashikiliwa na polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kumuua mumewe, Gwido Kigaya (59), kwa kumkata kwa panga kichwani. Tukio hilo lilitokea Machi 18, 2026 majira ya saa saba usiku katika kijiji cha Lwangu, baada ya kile kinachodaiwa kuwa ugomvi wa muda mrefu…
You May Have Missed
























