“Nitajizulu”: Waziri wa Nishati Zanzibar Atoa Kauli Katika Bunge la Wawakilishi

Waziri wa Maji, Nishati na Madini Zanzibar, Nadir Alwardy amesema yuko tayari kujiuzulu iwapo atashindwa kutekeleza majukumu yake na kuwatumikia wananchi ipasavyo.

Kauli hiyo ameitoa leo Mei 29, 2026 ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Maji, Nishati na Madini, huku akikiri kuwa wizara hiyo ni miongoni mwa wizara ngumu zaidi serikalini kutokana na changamoto zake kubwa.

Alwardy amesema hafanyi kazi kwa ajili ya kupenda vyeo bali kwa dhamira ya kutatua matatizo ya wananchi.

Na mimi niwaahidi, mimi siyo waziri ninayependa vyeo, nikishindwa kazi hii mimi nitajiuzulu,” amesema.

continue reading after ADVERTISEMENT

Siwezi mimi kukaa kwenye wizara kama siwezi kutumikia wananchi.”

Ameeleza kuwa amepewa dhamana hiyo kwa heshima kubwa na anaelewa matarajio yaliyopo kutoka kwa wananchi pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Nimesimama hapa kuwawakilisha wananchi, kukiheshimisha Chama Cha Mapinduzi,” amesema.

Hivyo nawaomba waheshimiwa wawakilishi wote waniamini, naenda kufanya kazi na nitakwenda kutatua changamoto zao. Sijaja hapa kufanya usanii ama kufurahisha watu.”

continue reading after ADVERTISEMENT

Waziri huyo pia amesema ni vigumu kuona matokeo makubwa ndani ya muda mfupi kutokana na uzito wa wizara hiyo na changamoto zake za muda mrefu.

Tangu nimekabidhiwa wizara hii ni miezi sita sasa. Wizara nzito sana na ndani ya miezi sita katika wizara hii huwezi kuona matokeo yake,” amesema.

Licha ya changamoto hizo, ameahidi kuendelea kushughulikia matatizo ya maji na umeme ambayo yamekuwa yakilalamikiwa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.

Kauli ya Alwardy imeanza kujadiliwa sana katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya wananchi wakisema si kawaida kwa viongozi wa kisiasa kutoa ahadi ya kujiuzulu hadharani iwapo watashindwa kutimiza wajibu wao.

continue reading after ADVERTISEMENT
READ  WHO Yaonya Ebola Kongo Inaweza Kusambaa Zaidi Afrika Mashariki

Wengine wameeleza kuwa kauli hiyo inaonyesha aina ya uwajibikaji ambao wananchi wengi wamekuwa wakiutaka kutoka kwa viongozi wa umma, hasa katika sekta zinazogusa maisha ya kila siku kama maji na nishati.

Changamoto za upatikanaji wa maji safi na huduma za umeme zimeendelea kuwa miongoni mwa masuala makubwa yanayogusa wananchi wa Zanzibar, hasa katika kipindi cha ongezeko la watu na ukuaji wa shughuli za kiuchumi na utalii visiwani humo.

RECOMMENDED FOR YOU
💬
ADVERTISEMENT ADVERTISEMENT