WHO Yaonya Ebola Kongo Inaweza Kusambaa Zaidi Afrika Mashariki

Shirika la Afya Duniani WHO limesema mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo huenda ulianza takribani miezi miwili iliyopita kabla ya kuthibitishwa rasmi.

WHO imesema tathmini ya ukubwa wa maambukizi pamoja na namna ugonjwa huo ulivyosambaa ndiyo imewafanya kufikia hitimisho hilo.

Hadi sasa watu zaidi ya 130 wamefariki dunia kutokana na mlipuko huo huku zaidi ya watu 600 wakishukiwa kuambukizwa ugonjwa huo hatari.

Mlipuko huo ulithibitishwa karibu wiki moja iliyopita katika jimbo la Ituri mashariki mwa Kongo.

continue reading after ADVERTISEMENT

WHO imesema idadi ya visa vya Ebola inatarajiwa kuendelea kuongezeka katika siku zijazo kutokana na kasi ya maambukizi iliyoripotiwa kwenye maeneo yaliyoathirika.

Shirika hilo pia limeonya kuwa kuna uwezekano wa maambukizi kusambaa kwenye nchi jirani na Kongo huku likizitaka mamlaka za afya kuongeza ufuatiliaji na tahadhari mipakani.

READ  Mfanyabiashara Apatikana Ameuawa Ndani ya Gunia Kenya, Watu Wanne Wakamatwa
RECOMMENDED FOR YOU
💬
ADVERTISEMENT ADVERTISEMENT