Leo Machi 17 2026 imetimia miaka mitano tangu kutokea kifo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano, Dr John Pombe Magufuli.
Daraja la Kigongo-Busisi, ni moja ya alama kubwa alizoziacha mioyoni mwa Watanzania ambapo akiwa hai aliwahi kueleza sababu iliyomsukuma kuchukua uamuzi wa kujenga daraja hilo, akisema aliguswa na tukio la ajali ya Mtumbwi iliyosababisha vifo vya Watu 11 katika eneo hilo.
Magufuli alipofariki Machi 17, 2021, ujenzi wa daraja hilo ulikuwa umefikia takribani asilimia 25 lakini baada ya kuingia madarakani, Rais Samia Suluhu Hassan aliendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo hadi ukakamilika na kuzinduliwa rasmi mwaka 2025, takribani miaka minne baada ya kifo cha Mtangulizi wake.
Miaka mitano tangu kuondoka kwa aliekuwa Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano, Dr John Pombe Magufuli






