Huduma za usafiri wa Anga katikati uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, Zimerejea rasmi siku ya Leo baada ya kuwa zimesitishwa kwa muda kufuatisha tukio la kungua kwa tanki lilokuwa likitumika kuhifadhi mafuta.
Moto huo uliripotiwa kusababishwa na shambulizi la drone, lakini Mamlaka zimethibitisha kuwa tukio hilo halikusababisha majeruhi wala uharibifu mkubwa ulioweza kuathiri shughuli za muda mrefu za uwanja huo.
Kwa mujibu wa taarifa za Mamlaka za United Arab Emirates, tukio hilo linatajwa kuwa shambulizi la tatu kulenga Uwanja huo tangu Iran ilipoanzisha mashambulizi ya kisasi dhidi ya mataifa ya Ghuba tarehe 28 Februari.
Wakati huo huo, shambulizi jingine la drone limeripotiwa kulenga miundombinu ya mafuta katika eneo la Fujairah, ambapo moto mkubwa ulizuka katika eneo la uzalishaji wa mafuta, huku Mamlaka za UAE zikisema juhudi za kuudhibiti moto huo bado zinaendelea







