Physical Address
Delta Corner Tower,
Waiyaki Way, Westlands, Nairobi, Kenya.
Contact us:
Email: info@todaysw.com
Physical Address
Delta Corner Tower,
Waiyaki Way, Westlands, Nairobi, Kenya.
Contact us:
Email: info@todaysw.com

Alphonce Felix Simbu, mwenye umri wa 33, ameandika historia kwa Tanzania baada ya kushinda medali ya dhahabu ya kwanza kabisa katika mashindano ya mbio za marathon โ World Athletics Championships โ yaliyofanyika Tokyo, Japan tarehe 15 Septemba 2025.
Mara ya mwisho Simbu alishinda medali kwa mashindano hayo ilikuwa mwaka 2017 London, ambapo alipata bronze kwenye marathon Sasa, ametinga kwenye chama cha wenye medali za juu zaidi.

Kwa ushindi huo, Tanzania imepata medali yake ya kwanza ya dhahabu kwenye mashindano ya dunia ya riadha, jambo ambalo limeitikisa nchi nzima. Simbu mwenye umri wa miaka 33 alisema kwa fahari, โLeo nimeandika historia, medali ya kwanza ya dhahabu kwa Tanzania.โ Machozi na tabasamu vilimchanganya huku akiangalia skrini kubwa ikithibitisha jina lake likiwa nafasi ya kwanza. Kwa upande wake Petros alikubali matokeo kwa maumivu na heshima, akisema hajawahi kuona marathon ikamalizika kwa kasi na ushindani kama huo, akilinganisha na mbio za mita 100.
Hili si tu ushindi wa mtu mmoja, bali ni ujumbe kwa taifa. Tanzania kwa miaka mingi imekuwa nyuma ya majirani zake kwenye riadha za umbali mrefu, mara nyingi ikibaki pembezoni wakati wenzetu wanatawala podium. Simbu ameonyesha kuwa hali hiyo inaweza kubadilika. Ushindi huu unaweza kuvunja ukuta wa kisaikolojia ambao umewazuia wanariadha wengi wa Kitanzania kuamini kwamba wana nafasi ya kupanda juu kabisa ya jukwaa la dunia.
Kwa jamii ya wanariadha, hili ni mwanga mpya. Inawezekana tukaanza kuona wawekezaji na wadau wakibadilisha mtazamo wao kuhusu michezo. Inawezekana pia vijana wa Kitanzania ambao wanakimbia barabarani kwa mazoezi ya kawaida sasa wakaamka kesho na ndoto kubwa zaidi, wakijua kuwa ndoto hizo si hadithi bali zinaweza kuwa kweli. Simbu ameandika historia, na historia hiyo sasa inamilikiwa na Watanzania wote.