Kikosi cha Yanga Sc kilicho chini ya Kocha Msaidizi wa timu hiyo Charles Mkwassa kimeanza safari leo kwa basi kuelekea Shinyanga kuifuata Mwadui FC.
Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara utapigwa Juni 13, Uwanja wa Kambarage.
Yanga Sc ipo nafasi ya tatu katika msimo wa ligi ikiwa na alama 51 baada ya kucheza mechi 27, huku Azam Fc ikiwa nafasi ya pili na wekundu wa msimbazi wakiwa nafasi ya kwanza.
Mwadui Fc ipo nafasi ya 12 baada ya kucheza mechi 28 ikiwa na jumla ya alama zake 34.
Licha ya Yanga Sc kupoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya KMC lakini bado wanayo matumaini makubwa ya kushinda mchezo dhidi ya Mwadui Fc, kadhalika Mwadui Fc nao wanasema wamejianda vizuri kuikabili Yanga Sc.
vyura