Burundi imempoteza mtoto wake wa kiume mwenye kustahili heshima, rais wa Jamhuri, kiongozi wa juu wa uzalendo wa taifa,” msemaji wa serikali Prosper Ntahorwamiye katika taarifa.

Nkurunziza, alieongoza taifa hilo dogo la Afrika Mashariki kwa mihula mitatu, alikuwa anapanga kustafu siasa baada ya uchaguzi wa Mei.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Nkurunziza, 55, alihudhuria mechi ya mpira wa wavu siku ya Jumamosi mchana na alipelekwa hospitali jioni hiyo baada ya kuugua.

Ingawa alionekana kupata ahueni siku ya Jumapili na kuzungumza na waliokuwa wamemzunguka, hali yake ilizidi kuwa mbaya ghafla siku ya Jumatatu asubuhi.

Kisha akapata mshtuko wa moyo na licha ya juhudi za haraka kuustua, madaktari hakuweza kumsaidia. Alifariki katika hospitali ya Natwe Turashoboye, mkoani Karuzi, mashariki mwa Burundi.

Rais Nkurunziza akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mkoani Gitega, katikati mwa Burundi, Aprili 27, 2020.

Serikali imesema kutakuwa na kipindi cha maombolezo cha siku saba kuanzia Jumanne na kwamba bendera zitapepea nusu mlingoti. Vitabu vya maombolezi vitakuwepo pia.

Nkurunziza aliingia madarakani mwaka 2005 baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya karibu watu 300,000. Vita hivyo viliwapambanisha watu wa jamii ya kabila la Wahutu walio wengi, dhidi ya Watutsi wachache.

Makubaliano ya amani ya Arisha yaliweka viwango vya ugawanaji wa madaraka, kwa lengo la kuwalinda Watutsi. Katika miaka iliyofuatia hata hivyo, chama tawala – Baraza la Taifa la Ulinzi wa Demokrasia – Vikosi vya Ulinzi wa Demokrasia (CNDD-FDD) – kilikuwa kimejitenga na masharti ya makubaliano hayo.

Wakati Nkurunziza, ambaye ni Mhutu, alipotangaza mwaka 2015, uamuzi wake wa kuwania muhula wa tatu, licha ya ukomo wa mihula miwili uliowekwa na makubaliano hayo, machafuko ya kiraia yalizuka.

Ushindi wake katika uchaguzi ukasababisha mzozo uliopelekea mamia ya watu kuuawa na mamia kwa maelfu wakaikimbia nchi.

2 thoughts on “Rais Nkurunzinza wa Burundi Afariki kwa Mshtuko wa Moyo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *