Marekani imetoa wito kwa serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na hatimaye kukamatwa kwa wale wote waliohusika na shambulio la kiongozi wa upinzani nchini humo Freeman Mbowe.
Mbowe alivamiwa na kushambuliwa na watu wasiojulikana wakati akirejea nyumbani kwake jijini Dodoma huku viongozi wa chama chake wakidai kwamba shambulio hilo lilishinikizwa kisiasa.
Kwa mjibu wa taarifa iliochapishwa katika tovuti ya ubalozi wake nchini Tanzania, imesema kwamba tukio hilo ni la kikatili na lisilo na sababu.

Taarifa hiyo ilisema

Ubalozi wa Marekani umeshtushwa na kuhuzunishwa na tukio la kikatili la kushambuliwa kwa mbunge na mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe tarehe 9 Juni, tunatoa pole kwa mbunge huyo na familia yake


Ubalozi wa marekani umesema shambulio la kiongozi huyo wa Chadema ni miongoni mwa matukio ya kusikitisha ya utumiaji wa nguvu na unyanyasaji yanayofanywa dhidi ya wanachama wa vyama vya upinzani.
Aidha ubalozi huo umetambua kwamba mojawapo ya mashambulio hayo ya kikatili dhidi ya viongozi wa upinzani ni jaribio la mauaji lililotokea tarehe 7 mwezi Septemba 2017 dhidi ya Tundu Lissu ambalo ufumbuzi wake haujapatikana hadi leo.
Kwa sasa kiongozi huyo wa Chadema anaendelea kupata matibabu katika moja ya hospitali zilizopo jijini Dodoma.

One thought on “Marekani yaitaka Tanzania kuwakamata wote waliomshambulia Freeman Mbowe”
  1. mavi yule hajadhambuliwa wala nini au hukusikiloza bunge jana nini¿?..yule aliteleza sema acting ka zote yani😪😪

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *